BAADHI YA VIONGOZI KAUNTI YA KILIFI WALAANI KISA CHA KUPIGWA RISASI KWA MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA ENEO LA MIGINGO

Kufuatia kisa cha kupigwa risasi kwa Mbaga Lewa mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Maziwani siku mbili zilizopita kwenye mzozo wa ardhi eneo la Migingo mjini Malindi baadhi ya viongozi katika kaunti hii wamewalaani maafisa wa polisi
Kuhusiana na kitendo hicho.

Wakiongozwa na Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi wanadai kwamba tukio hilo limetekelezwa kinyume cha sheria na sharti swala hilo lifikishwe kwa mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa polisi IPOA na kuahidi kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha familia ya kijana huyo inapata haki.

Ni Kauli ambayo imeungwa mkono na mwakilishi wa wadi ya Malindi Town David Kadenge Dadu na kuongeza kuwa polisi walitumia nguvu kupita kiasi kwenye tukio hilo na kumtaka inspekta Jenerali wa polisi nchini Hillary Mutyambai kuchunguza vyema bunduki iliyotumika kutekeleza kitendo hicho ili hatua za sheria zichukuliwe dhidi ya muhusika.

Haya yanajiri huku mwanafunzi huyo akiendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Malindi kaunti ya Kilifi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.