Vijana Magarini walalamikia kukosa kazi katika mpango wa kazi mtaani

Mwanaharakati wa maswala ya vijana katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Gracious Nyamawi ambaye pia ni mmoja wa walio katika bunge la mwanachi ameelezea kuwepo kwa hali ya sintofahamu katika kuajiriwa kwa vijana kwa mradi wa kazi mtaani.
Nyamawi amehoji kuwa hakujakuwa na uwazi katika kuajiriwa kwa vijana hao na hii ni baada ya baadhi ya vijana kukosa kuhusishwa kikakamilifu baada ya kutuma maombi ya kupata kazi hiyo.
Nyamawi ameongeza kuwa baada ya kutafuta kujua mwafaka wa swala hilo walibaini kuwa zipo baadhi ya sehemu ambazo ziliteuliwa kuwa sehemu za kazi jambo ambalo liliwalazimu kuwateua vijana kutoka eneo la Gongoni na Mamburi ikifahamika kuwa sehemu hizi zipo katika wadi mbili pekee.
Aidha mwana harakati huyo amewataka maafisa wanaowasimamia vijana kuwa na usawa katika shughuli za kuwaajiri vajana kwani mpango kwa kazi kwa vijana ulinuia kuwafaidi vijana wote katika wadi zote zilizoko katika eneo bunge la Magarini na wala sio Gongoni pekee.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.