Vijana Kadzandani kaunti ya Mombasa walalamikia kubaguliwa kwenye miradi mbali mbali

 

Mkurugenzi wa shirika la vijana la Kadzandani Creative Omar Chai amesema vijana eneo la Kadzandani kaunti ya Mombasa hadi kufikia sasa hawajanufaika na miradi muhimu ambayo inaidhinishwa na serikali kutokana na ukosefu wa maafisa tawala wa sehemu hiyo.
Kwa sasa muda wa saa 24 umetolewa kwa idara ya usalama sambamba na serikali ya kaunti hiyo kupeleka Chifu, Naibu wake pamoja na msimamizi wa wadi katika eneo la Kadzandani eneo bunge la Nyali.
Ameongeza kuwa ukosefu wa maafisa tawala umechangia pakubwa kwa vijana eneo hilo kubaguliwa kwenye miradi inayoidhinishwa na serikali kuu na ya kaunti ya Mombasa.
Hata hivyo ameongezea kwamba mradi wa kazi mtaani umekosa kuwafaida vijana wa Kadzandani kutokana na kile ambacho wanadai kubaguliwa na chifu wa Kisimani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.