Ukame wa magoli haumnyimi usingizi Mo Salah

Februari 9 mwaka huu dhidi ya Bournemouth, ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Mo Salah kuifungia goli Liverpool. 
Hiki ndio kipindi kirefu kwa Mo Salah kucheza bila kuifunga goli akiwa Liverpool.

Baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Tottenham Mo Salah amesisitiza kuwa hajali hata kidogo kutokufunga kama timu yake inaondoka na ushindi.

Salah jana alifanya kazi kubwa katika upatikanaji wa goli la ushindi ambapo mpira wa kichwa alioupiga katika dakika ya 90 ulifanya beki wa Spurs Toby Alderweireld kujifunga. 
.
“Sijafunga kwa mechi chache na kuna wachezaji wenye magoli sawa na mimi na wanasema (huu) ndio msimu wao bora katika maisha yao” Salah alimwambia beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher katika kituo cha Televisheni cha Sky Sports. 
.
‘Sijali kama sijafunga goli, pointi tatu ndio kitu muhimu’ alisisitza mchezaji huyo kutoka Misri.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.