UHaba wa umeme waendelea kushuhudiwa eneo la Moi kunti ya Kilifi

Wakaazi wa eneo la Moi, Sabaki kaunti ya Kilifi wamelalamikia ukosefu wa umeme kwa muda wa miaka mitatu sasa huku wakiitaka serikali kuhakikisha kuwa inawapatia huduma hiyo muhimu.
Wakiongozwa na msemaji wao Safari Kadenge wanadai kuwa ukosefu huo katika eneo hilo umechangia pakubwa utovu wa usalama sawia na uvamizi wa wanyamapori wakiwemo viboko ambao huvamia makazi yao nyakati za usiku jambo linalohatarisha maisha ya wakazi.
Wanasema kuwa tangu mradi huo ulipoanzishwa miaka mitatu iliyopita haujakamilishwa hadi kufikia sasa kwani ni milingoti tu ya umeme iliyowekwa bila nyaya za kupitisha nguvu za umeme huku wakihofia kuwa huenda mradi huo usikamilike kufuatia janga la korona.
Aidha wamelalamikia vikali mkandarasi aliyepewa jukumu la kuendeleza mradi huo wakisema kuwa amezembea katika utendakazi
Kwa Sasa wanaitka serikali kupitia viongozi wa eneo hilo kuingilia kati swala wakisema kuwa viongozi wengi wameelekeza jitihada zao katika janga la Corona huku miradi mingine muhimu ya wananchi ikiwachwa nyuma.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.