Tyson Fury amtoa povu Braun Strowman kwenye pambano la WWE Crown Jewel

Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Tyson Fury sasa amekuwa Superstar asiyeshindikana wa WWE, baada ya pambano lake jana.

Mazoezi yake ya wiki nne ya kujenga misuli na kujiandaa na pambano lake dhidi ya jitu la miraba saba Braun Strowman almaarufu kama ‘Monster Among Men’ yamelipa baada ya kumpatia kichapo cha mbwa kwenye pambano la Crown Jewel lililofanyika jana huko Riyadh, Saudi Arabia.

Pambano hilo lililotaliwa na tambo na kutupiana meneno ya kejeli na vijembe, lilimshuhudia Fury akijitupa ulingoni kwa tambo zote kuanzia mwanzo hadi mwisho kuwa atanyakua ushindi kwenye pambano ambalo linaripotiwa kumuingizia £12m.

Hata hivyo mwanzoni mwa pambano Fury alipokea kichapo kidogo lakini mwisho alionesha ubabe wake kwa kumpiga Strowman kichwani kwa mkono wake wa kulia wakati anarudi ulingoni.

Baada ya mechi Fury hakutaka kusema kama atarejea tena kwenye WWE, lakini alisema anataka kushughulikia mechi yake na bingwa wa uzito wa juu duniani wa WBC Wilder, iliyopangwa kufanyika Februari 22.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.