TUTAWANYUKA KANGEMI ALL STARS 5-0, SHABIKI WA YOUNG BULLS ASEMA

Popote kambi, nyumbani kambi ugenini kambi

Ni kauli yake shabiki sugu wa klabu ya young bulls wasi dante ambaye anaamini kwamba klabu hiyo itazoa ushindi wa magoli 5-0 kwenye mechi yao ijayo dhidi ya kangemi all stars jijini nairobi.

‘’Mimi popote kambi, home kambi na nikija kwako pia ni kambi. Najiamini bwana. Si leo tumewachapa nne. Tukienda kwao pia tutazidisha ziwe tano. Wataitana. Mchezo uko Coast bwana,’’ alisema Dante.

Kwenye mechi yao ya kwanza ya ligi ya kitaifa daraja la kwanza BETKING DIV ONE LEAGUE Young Bulls waliwacharaza Ruiru Hotstars  ya kaunti ya Kiambu magoli 4-0 katika dimba la Alaskan mjini Malindi kaunti ya Kilifi.

Ni mara ya kwanza kwa klabu ya Bulls  kushiriki michuano hii na tayari wameonyesha tumaini la kung’ara hata zaidi kwenye michuano ya kitaifa.

Kwa mjibu wa afisa wa michezo wa kaunti wa eneo la kaunti ndogo ya Magarini na Malindi ni kuwa Young Bulls wako vizuri na wataenda mbali endapo watawekeza katika mazoezi zaidi pamoja na kuwa na ushirikiano wa kina.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Elvis Baya, Melda ameihimiza jamii kukumbatia swala la talanta miongoni mwa vijana kwa kuwa kaunti haijafika kiwango cha kusaidia vilabu vyote asilimia mia.

Amewataka wadhamini na wahisani kujitokeza kusaidia ukuaji wa vipaji lakini pia kuwaomba wawekezaji kuingia kwenye mikataba na vilabu vya mashinani kwani ni kupitia kufanya hivyo vilabu vitainuka na kuinuka kwa vilabu ni ufanisi wa wachezaji na kuinuka kwa jamii kwa ujumla.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.