Tunaweza kuisaidia Afrika pasipo masharti, asema Putin

Raisi wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa nchi yake inaweza kuisaidia Afrika bila masharti ambayo huambatanishwa kwenye misaada ya mataifa ya magharibi.

Putin ameeleza katika mahojiano na shirika la habari la Urusi TASS, kabla ya mkutano na viongozi wa Afrika. Urusi inatarajia kuwa mwenyeji wa viongozi 47 wa Afrika katika mkutano wa tarehe 23 -24 mwezi Oktoba mjini Sochi.

Putin amesema mahusiano na Afrika yemeimarika, akiainisha makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya silaha, ambapo Urusi imefanikiwa kushawishi mataifa zaidi ya 30 kuwasambazia silaha.

Rwanda ni moja ya nchi ambazo zimekuwa na mahusiano mazuri sana na Urusi. Baraza la mawaziri la Rwanda hivi karibuni liliridhia makubaliano na urusi katika masuala ya matumizi ya nishati ya nyukilia kwa ”matumizi ya amani”,

Teknolojia hii itatumika katika uzalishaji wa nishati na utunzaji wa mazingira.

Marekani imekuwa ikipoteza ushawishi barani Afrika- lakini mwanadiplomasia wa juu wa nchi hiyo barani Afrika anataka kubadili hali hiyo.

Trump alishawahi kuripotiwa kuyataja mataifa ya kiafrika kuwa ni ”nchi chafu” na kuongelea Afrika kama sehemu ambayo marafiki zake wanakwenda kujaribu kutajirika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.