Tume ya EACC yatakiwa kuwajibikia majukumu yake ipasavyo

Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURU Khelif Khalifa amesema hakukuwa na ulazima kwa rais Uhuru Kenyatta kuamrisha uchunguzi kuhusiana na sakata ya ufujaji wa fedha ambazo zilikuwa zimetengwa ili kukabiliana na janga la Corona.
Katika taarifa yake mwenyekiti huyo amesema kwamba tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC sambamba na idara ya upelelezi DCI zilipaswa kushughulikia uchunguzi huo bila kusubiri maagizo kutoka kwa rais kwa kuwa ni jukumu la taasisi hizo kufanya uchunguzi huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.