TAKRIBANI WATU 15 WAPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI MBAYA YA BARABARANI

Watu 15 wamethibitishwa kuaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani  ambayo imetokea katika eneo la Kwa Shume, barabara kuu ya Mombasa Malindi mwendo wa saa moja asubuhi.

Kamishina wa Kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka amesema watu 14 wameaga papo hapo huku mmoja akiaga dunia wakati alipokuwa akiendelea kupata huduma za matibabu Hospitalini.

Hata hivyo Olaka amebainisha kuwa mpaka sasa hawajapata idadi kamili ya majeruhi katika ajali hiyo iliyohusisha gari la Muhsin iliyokuwa ikielekea Garsen kutoka Mombasa na Sabaki Shuttle iliyokuwa inaelekea mjini Mombasa kutoka Malindi.

Olaka amewataka madereva kuwa waangalifu zaidi wakati wanapokuwa barabarani.

baadhi ya walionusurika wanaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali kuu za mjini Malindi na Kilifi huku Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi akiwa  miongoni mwa viongoizi katika kaunti hii ambao wametuma risala za rambi rambi kwa waliowapoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo.

 

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.