Swamad azindua awamu ya pili ya zoezi la kupima wenyeji virusi vya Corona

 

Mbunge wa Mvita kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amewarai wenyeji kujitokeza na kufanyiwa vipimo kubaini ikiwa wameambukizwa virusi vya Corona au la.
Akizungumza katika Mji Wa Kale huko Mombasa kwenye awamu ya pili ya uzinduzi wa zoezi la kuwapima wenyeji virusi hivyo Swamad amewataka wenyeji kuondoa hofu kuhusu vipimo hivyo na kuongeza kuwa hatua ya kuwapima itawawezesha wakaazi hao kutambua hali zao za kiafya.
Ni zoezi ambalo limeratibiwa kufanyika kwa muda wa wiki moja maeneo ya Mwembe Tayari, Mji Wa Kale, Tudor na Mvita huku akiwataka wenyeji kuendelea kuzingatia maagizo yanayotolewa na serikali kupitia wizara ya afya ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.