Swale Simba apinga madai ya kutaka kumbandua mamlakani Gavana Salim Mvurya

Mwakilishi wa wadi ya Tsimba/Golini kaunti ya Kwale Swaleh Simba amekanusha vikali madai ya kumbandua mamlakani gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya.
Akiongea mjini Kwale, Simba amekanusha madai ya kutia saini hoja ya kutokuwa na imani na uongozi wa serikali ya kaunti ya Kwale.
Mwakilishi huyo amesema mchakato wa kumbandua Mvurya umechochewa kisiasa na baadhi ya viongozi wa kaunti hiyo huku bunge la kaunti ya Kwale likikanusha tayari madai ya kuwasilisha hoja la kumng’atua gavana Mvurya.
Hata hivyo, Simba ameahidi kuunga mkono azma ya naibu wa gavana wa Kwale Fatuma Achani ya kutaka kuwania kiti cha ugavana mwaka wa 2022.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.