SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA KILIFI AKINZANA NA HATUA SRC KUPINGA RUZUKU YA MAGARI

Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi, Jimmy Kahindi amekinzana na hatua ya msimamizi mkuu wa bajeti ya serikali Margret Nyakang’o kwa kupinga ruzuku ya magari iliyopaniwa kufikia maspika wa mabunge ya kaunti sawia na wawakilishi wa wadi.

Kahindi amesema kuwa idara husika za serikali zilihusika katika kutoa uamuzi wa ruzuku hiyo hivyo ni sharti serikali iingilie kati katika swala hilo kwani tume ya kutathmini mishahara ya wafanyikazi wa umma, SRC ilikuwa miongoni mwa idara zilizohusika katika kuhakikisha kuwa ruzuku hiyo inafanikishwa.

Spika huyo ameeleza kushangazwa kwake na kusimamishwa kwa harakati hizo kwa kile alichosema kuwa haoni sababu mwafaka zinazopelekea ruzuku hiyo kutofanikishwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.