soko jipya Oloitiptip mjini kilifi latarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi uajo

Serikali ya kaunti ya kilifi imejenga soko jipya litakalo wasaidia wafanyibiashara kuimarisha hali yao ya kiuchumi katika soko la Oloitiptip mjini kilifi ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi ujao.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Michael Kilumo amesema kuwa, usafi, usalama na hadhi ya soko hilo utachangia pakubwa kuinua   uchumi Kwa wafanyibiashara hao ambapo hapo awali wamekuwa wakishindwa kufanya biashara zao kutokana na hali duni katika soko hilo.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa bodi ya Manispaa mjini kilifi Charles Ngala asema kuwa soko hilo limejengwa kwa kiwango cha kimataifa la masoko na linatarajiwa kufunguliwa mapema mwezi ujao.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.