Shirika la umoja wa afrika NEPAD LAANZISHA ZOEZI LA kutathmini utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini

Zoezi la kutathmini utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini kupitia serikali za kaunti limeanzishwa na Shirika la umoja wa Afrika NEPAD.
Mkurugenzi wa shirika hilo Elias Mbau aliyekuwa akizungumza na wanahabari baada ya kukutana na gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema zoezi hilo litawezesha taifa hili kujumuika na nchi za Afrika katika masuala ya utatuzi wa changamoto zinazokumba bara la afrika katika misingi ya kimaendeleo.
Aidha amezitaka serikali za kaunti kukubali ukaguzi wa mahesabu ya utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika serikali za kaunti kama vile serikali ya kitaifa inavyofanya.
Hata hivyo gavana wa Kwale Salim ameunga mkono zoezi hilo akisema kwamba linalenga kuacha kumbukumbu ya serikali za kaunti zinavyotekelezwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.