shilingi milioni 220 kutumika kununua madawa na vyakula kwa familia zilizoathirika kiuchumi Kilifi

 

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amesema kwamba amemaliza siku 14 ambazo amekuwa kwenye karantini na baada ya vipimo hajapatikana akiwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwa mara ya kwanza baada ya kutoka kwenye karantini Kingi ameelezea mikakati ambayo imewekwa na serikali ya kaunti ya Kilifi katika kuhamasisha umma kuhusu ugonjwa wa Covid- 19.
Amehoji kwamba Wananchi ambao biashara zao zimepigwa marufuku wameorodheshwa kama baadhi ya wakazi watakaopewa kipau mbele katika mchakato wote wa kupewa msaada wa kifedha na chakula.
Vile vile Kingi amesema bunge la kaunti ya Kilifi liko katika harakati za kupitisha bajeti ya ziada ya takribani shilingi milioni 220 ambazo zikipitishwa zitalenga kununua madawa na vyakula kwa familia zilizoathirika pakubwa kiuchumi kutokana visa vya virusi vya korona kaunti ya Kilifi.

1 thought on “shilingi milioni 220 kutumika kununua madawa na vyakula kwa familia zilizoathirika kiuchumi Kilifi”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.