Shilingi milioni 10 zatumika kununua Ng’ombe 58 wa maziwa kaunti Kilifi

 

Kima cha shilingi milioni 10 zimetumika na serikali ya kaunti ya Kilifi kununua Ng’ombe 58 wa maziwa ambao waligawanyiwa makundi mbali mbali ya wenyeji wa wadi ya Ganda eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi.
Mwakilishi wa wadi hiyo Reuben Katana Mwamure, amesema lengo la mradi huo ni kuhakikisha uchumi wa eneo hilo unaimarishwa sambamba na kuinua hali ya maisha ya wakaazi hao.
Hata hivyo, ametoa wito kwa wakaazi walionufaika na mradi huo kuhakikisha kuwa wanazingatia elimu waliyopewa na wataalam wa ufugaji kuhusu mbinu za kuwafuga Ng’ombe hao ikiwemo kuwadunga sindano na pia kuwaweka katika mazingira safi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.