Serikali yatakiwa kuboresha miundo msingi shuleni

 

Katibu wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET tawi la Kwale Mackenzie John Ntuki ameitaka serikali kuboresha miundo msingi katika shule za upili i;i wanafunzi wapate elimu katika mazingira yaliyobora.
Ntuki amesema licha ya wazazi kuzingatia amri ya wazazi kuhakikisha watoto wao waliomaliza darasa la 8 wanajiunga na kidato cha kwanza ni kwamba serikali imefeli katika kuziimarisha shule za umma.
Kwa mujibu wa katibu huyo ni kwamba ni jukumu la serikali kuhakikisha madarasa yanajengwa sambamba na kupelekwa vifaa vingine muhimu na kusema iwapo hayo hayatatekelezwa msongamano wa wanafunzi utaendelea kushuhudiwa katika shule za umma nchini.
Hata hivyo ameongeza kwamba ili kuboresha sekta ya elimu nchini ni lazima serikali kupitia tume ya SRC inawaajiri walimu zaidi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.