Serikali yashutumiwa kwa kuwahangaisha wenyeji wa pwani

Afisa wa maswala ya dharura katika shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la MUHURI Francis Auma amewataka wenyeji wa kanda ya pwani ambao wamekuwa wakifurushwa kwenye makazi yao wakati huu wa kukabiliana na janga la Corona kutoyahama maeneo hayo.
Auma amesema wenyeji hawatavumilia dhuluma hizo ambazo zimekuwa zikiendelezwa kwa muda sasa na kuongeza kuwa serikali haina mamlaka ya kuwahangaisha wakenya na ni lazima wananchi wasimame kidete katika kutetea haki zao.
Hata hivyo, ameitaka serikali kukoma kuwahangaisha wenyeji wakati huu hali ngumu ya maisha inaendelea kuwakumba.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.