SERIKALI YA KAUNTI YA TAITA TAVETA YATAKIWA KUWA NA UWAZI KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

Mashirika ya kijamii katika kaunti ya Taita Taveta sasa yameitaka serikali ya kaunti hiyo kuwa na uwazi katika matumizi ya fedha za umma hasa fedha zilizotengwa kukabiliana na janga la virusi vya corona.
Mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu la Taita Taveta Human Rights Watch Haji Mwakio, amelaumu viongozi na taasisi husika kwa kutowajibika ipasavyo katika maswala ya fedha kwa kile anachodai kuwa kimeshinikizwa na uongozi mbaya.
Ni kauli iliyoungwa mkono na shirika la Uraia Trust likiungama kuwa uongozi mbaya katika serikali ya kaunti ya Taita Taveta, umepelekea wakaazi kukosa huduma muhimu ikiwemo ya afya na kukabiliana na ugonjwa wa covid 19.
Aidha mashirika hayo sasa wanashinikiza  taasisi na idara husika kuweka wazi ripoti ya mipangilio na matumizi ya fedha zinazotolewa ili kuwe na uwazi na uwaajibikaji wa matumzi ya fedha za umma.
Mashirika hayo yanasema kuwa licha ya kuwasilisha malalamishi ya matumizi mabaya ya fedha za covid 19 bunge la kaunti hiyo halijaweka wazi matokea ya uchunguzi wake wala ripoti kamili ya jinsi fedha zilizotengewa covid 19 zilitumika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.