SERIKALI YA KAUNTI YA LAMU YATAKIWA KUTUMIA VYANZO VYA MAJI KUDHIBITI UHABA WA MAJI

Afisa wa shirika la Haki Afrika kaunti ya Lamu Yunus Ahmed Is’hakia ameitaka serikali ya kaunti hiyo kutumia vyanzo vya maji katika kaunti ya Lamu ili kudhibiti uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo .
Yunus amesema kuwa hatua ya serikali ya kaunti hiyo kuendeleza miradi ya kuweka mashine za kubadilisha maji chumvi kuwa maji tamu sio suluhu la kudumu katika kukabiliana na tatizo hilo la maji katika kaunti ya Lamu.
Ameongeza kwamba ni mashine ambazo zinatumia fedha nyingi ili kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara huku akidai haziwezi kutoa kiwango cha maji ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya wenyeji wote.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.