Serikali ya kaunti ya Kilifi yapiga marufuku hudumu za boda boda ili kudhibiti Corona

 

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amesema serikali ya kaunti ya Kilifi imechukua hatua zaidi kwa kupiga marufuku hudumu za boda boda kwa wateja kama njia moja ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika taarifa yake Kingi amewataka whudumu wa tuk tuk kuhakikisha wanambeba abiria mmoja pekee na kuwaagiza wamiliki wa maduka ya kawaida ya yale ya jumla ambayo hayauzi bidhaa muhimu kufunga biashara zao.
Vile vile ameagiza kufungwa kwa viwanda ambavyo vina wafanyikazi wengi huku serikali ya kaunti ya Kilifi ikisema inafuatilia kwa ukaribu swala la kudumiswa kwa usafi katika masoko na iwapo yatakiuka kanuni za usafi basi yatalazimika kufungwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.