SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI KUIMARISHA MIUNDO MSINGI YA BARABARA

Mwakilishi wa Wadi ya Garashi kaunti ya Kilifi Peter Ziro amesema Serikali ya Kaunti hii itaendelea na juhudi za kuimarisha miundo msingi ya barabara ili kurahisisha usafiri kwa wakaazi wake.
Ziro amehoji kuwa tayari kima cha Shillingi Millioni 15 zimetengwa kwenye Bajeti  ili kuzikarabati upya barabara za kaunti ya Kilifi, ili kurahisisha usafiri wa Wafanyibiashara wadogo wadogo.
Ameongeza kuwa tayari wamekubaliana na wakaazi eneo hili kuangazia zaidi swala la Barabara na maji katika Bajeti ya mwaka wa 2021-2022.
Amepongeza juhudi za Serikali ya Kaunti hii katika jitihada za kusambaza maji safi kwa wakaazi huku akibainisha kwamba, uharibifu wa mabomba ya maji katika baadhi ya sehemu ndiyo imekuwa changamoto kubwa inayochangia kwa baadhi ya maeneo kukosa bidhaa hiyo muhimu, akisisitiza haja ya baadhi ya mabomba hayo kubadilishwa.
Hata hivyo Ziro amesema tayari wametenga Shillingi Millioni kumi ili kushughulikia swala la Maji huko Garashi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.