Sekta ya bodaboda ina uwezo wa kuimarisha maisha ya vijana, Juma Thoya asema

Mwakilishi wa wadi ya Mikindani, katika kaunti ya Mombasa Juma Renson Thoya amesema sekta ya boda boda ina uwezo wa kunufaisha maisha ya vijana sawia na sekta zingine.

Thoya amesema kuwa sekta hiyo ikipata usimamizi mzuri na kuboreshwa basi vijana wengi watapata nafasi ya kujiajiri katika sekta hiyo jambo litakalochangia ukuaji wa uchumi katika kaunti hiyo.

Mwakilishi wadi huyo amesema kuwa vijana wengi hujihushisha na visa vya uhalifu kutokana na ukosefu wa ajira huku akiongeza kuwa vijana wanapaswa kupewa mbinu za kujiajiri ili kujikimu kimaisha.

Thoya amesema haya alipokuwa akikabidhi pikipiki mbili kwa kundi moja la wahudumu wa bodaboda.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wahudumu wa bodaboda huko Bangladesh Joseph Nyaberi amekiri kuwa vijana wengi wamenufaika pakubwa katika sekta hiyo huku akiwataka wanabodaboda katika eneo hilo kutojihusisha na maswal a ya utovu wa usalam ili kujenga taswira njema ya sekta hiyo ikizingatiwa kuwa jamii imeweka mtazamo tofauti kuhusu wahudumu wa bodaboda.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.