SALMA HEMED ADAI WAZAZI KUWATELEKEZA WATOTO WAO

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limesema kuwa utepetevu katika malezi miongoni mwa wazazi umechangia kupotoka kimaadili kwa watoto wengi kaunti ya Mombasa.

Naibu mkurugenzi wa shirika hilo, Bi. Salma Hemed amesema kuwa wazazi wengi hawana muda wa kutoa mwelekeo ufaao kwa watoto wao jambo linalowapelekea vijana wengi kukumbwa na masaibu mbalimbali.

Bi. Salma amesema ni sharti wazazi watekeleze majukumu yao ya kuwaongoza watoto wao katika mienendo na maadili yanayopaswa ili kuwaimarisha kimaisha.

Mwanaharakati huyo ameitaka jamii kushirikiana katika malezi ya watoto huku akiwataka kuondoa dhana kuwa kila mzazi anapaswa kushughulikia mwanawe pekee kwani vijana wanaojitosa katika utovu wa usalama huathiri jamii nzima kwa jumla.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.