Ruweida Obo awataka wanasiasa lamu kuweka kando maswala ya siasa

 

Viongozi katika kaunti ya Lamu wametakiwa kuweka kando maswala ya siasa na badala yake kuwahudumia wananchi wakati huu taifa linakumbwa na janga la Corona.
Akitoa wito huo mwakilishi wa kike katika kaunti hiyo Ruweida Obo amesama wakati huu visa vya virusi hivyo vinazidi kushuhudiwa ipo haja ya viongozi kuungana katika kulikabili janga hilo.
Ruweida amesema serikali kuu na wizara ya afya katika kaunti hiyo zitaendelea kushirikiana ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.
Ameyazungumza haya baada ya kutoa msaada wa Hema na vifaa vya kupima joto eneo la Witu, Mtangawanda, Kizingitini na Kiungana ili kusaidia kudhibiti Covid-19.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.