Ramadhan Seif Kajembe aaga dunia

 

Aliyekua Mbunge wa Changamwe kaunti ya Mombasa Ramadhan Seif Kajembe ameaga dunia katika Hospitali ya Pandya mjini Mombasa.

Kifo cha Kajembe kinajiri wiki mbili tu baada ya mke wake wa kwanza Aziza Kajembe kufariki kutokana na kile kinachisemekana alikuwa anaugua Covid-19 na Mwezi Machi mwaka huu mke wake wa pili Zaharia Kajembe aliaga dunia.

Mwenda zake Kajembe alihudumu kama mbunge wa Changamwe kati ya mwaka wa 1997 na mwaka 2007 kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na mbunge wa sasa Omar Mwinyi ambaye alishinda kiti hicho mwaka wa 2013.

Viongozi mbali mbali akiwemo kinara wa chama Cha ODM Raila Odinga kupitia ujumbe wake wa Twitter ni miongoni mwa wale ambao wametuma risala zao za rambi rambi na kumtaja kama kiongozi aliyekuwa amejitolea katika kuwahudumia wenyeji na pia taifa la Kenya kwa ujumla.

Kifo cha Kajembe hakijabainika japo anadaiwa alikuwa na dalili za virusi vya Corona.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.