Rais Kenyatta ahimizwa kutangaza mimba za utotoni kama janga la Kitaifa

Huku swala la mimba za mapema likiendelea kuibua hisia mseto katika kaunti ya Kilifi na taifa la Kenya kwa jumla viongozi katika kanisa la ACK mjini Malindi katika kaunti ya Kilifi wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kutangaza swala hilo Kama janga la kitaifa.
Wakiongozwa na Askofu Lawrence Dena katika kikao na wanahabari mjini Malindi wamesema kuwa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wale walioathirika na visa hivyo ni wanarika walio na umri wa kati ya miaka 10 – 14 huku kaunti ya Nairobi ikiongoza kwa visa elfu Kumi na viwili.
Hata hivyo, Askofu huyo ametaja wahudumu wa boda boda Kama watu ambao wamekuwa wakichangia Zaidi katika kuwapachika mimba watoto hao hasa wakati huu ambapo wako majumbani kutokana na ugonjwa wa Covid-19.
Aidha, Askofu huyo amesema kuwa suluhu la kupambana na janga la visa vya mimba za mapema ni kuhakikisha kuwa watoto wanafunzwa masomo ya kidini jambo litakalo wawezesha kukua kimaadili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.