RAILA ODINDA ASEMA HAKUNA MAPENDEKEZO ZAIDI YATAKAYOJUMUISHWA KWENYE RIPOTI YA BBI

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amehoji kuwa hakuna mapendekezo zaidi ambayo yatajumuishwa kwenye ripoti ya BBI.
Katika taarifa yake baada ya kukutana na viongozi wa baraza la kitaifa la ushauri wa waislamu chini KEMNAC kinara huyo wa ODM amesema kuwa ripoti hiyo itaendelea kufanyiwa marekebisho baadae lakini sio sasa.
Haya yanajiri baada ya viongozi wa baraza hilo kudai kuwa maswala mengi yanayohusu waumini wa dini hiyo kukosa kujumuishwa kwenye ripoti ya BBI..
Wakato uo huo mwenyekiti wa baraza hilo la KEMNAC Sheikh Juma Ngao ameeleza imani yake kuwa baadhi ya mapendekezo ambayo yaliwasilishwa kwa kinara huyo wa ODM Raila Odinga yatajumuishwa katika ripoti ya mwisho ya BBI.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.