RAILA ASEMA BBI ITAFANIKISHA SWALA LA USAWA WA JINSIA UONGOZINI

Mikutano ya kisiasa imeendelezwa na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga katika maeneo mbali kwenye kaunti ya Mombasa.
Kwenye hotuba yake katika eneo la Chagamwe amewarai wenyeji wa kaunti ya Mombasa na ukanda wa pwani kwa jumla kuunga mkono mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho kupitia muswada wa BBI.
Raila ameongeza kuwa ni kupitia kuidhinishwa kwa BBI ndipo swala la usawa wa Jinsia uongozini litafanikishwa na kuwanufaisha vijana na kina mama.
Hotuba ya kinara huyo wa ODM imetatizwa na wafuasi wa mwanasiasa na pia mfanyabiashara Suleiman Shahbal na wale wa Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir ambao wanapania kuwania kiti cha ugavana kwenye kaunti ya Mombasa hali ambayo imemlazimu gavana wa kaunti hiyo Ali Hassan Joho kuingilia kati ili kuwatuliza wafuasi hao.
Ni fursa ambayo Gavana Joho ametumia kujipigia deba katika azima yake yakuwania urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Raila amesema kuwa Joho ana haki ya kuwania kiti hicho kwani chama cha ODM kinaunga mkono maswala ya kidemokrasia.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.