Nyota ya Olunga yazidi kung’aa Japan

Mshambuliaji matata wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Michael Olunga ambaye anachezea timu ya Kashiwa Reysol ya Japan amefunga goli la kufutia machozi wakati timu yake ilipokubali kichapo cha magoli 2 – 1 kutoka kwa Sagan Tosu katika mechi ya Ligi Kuu ya Japan.

Olunga kwa sasa analiongoza jedwali la wafungaji bora wa Ligi hiyo kwa magoli 16 kutokana na mechi 15.

Bao lake Olunga dhidi ya Tosu lilipatikana katika dakika ya 24.

Ushawishi wa Olunga unazidi katika kambi ya Reysol tangu aongoze kikosi hicho kupanda ngazi na kufikia Ligi Kuu mwishoni mwa msimu uliopita 2019/2020.

Katika mchuano wa mwisho ulioshuhudia Reysol wakiwapiga Gamba Osaka 3-0 ligini, Olunga alipachika wavuni bao la kwanza katika dakika ya pili na kufikisha jumla ya magoli 15 kapuni mwake.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.