NCIC yapendekeza kupewa nguvu zaidi

 

Vikao rasmi vya kupokea mapendekezo kutoka kwa taasisi na watu binafsi vimeanzishwa rasmi na kamati ya maridhiano ya BBI ili kubaini yanayotakiwa yajumuishwe katika ripoti hiyo.
Ndicho kikao cha kwanza cha kamati hiyo baada ya rais Uhuru Kenyatta kuongezea muda na BBI kuchapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali.
Kamati hiyo imekutana na tume ya uwiano na maridhiano NCIC chini ya mwenyejiti wake Kasisi Samuel Kobia huku akiitaka ipewe nguvu za kuwashtaki na kuwaadhibu watu wanaopatikana kuwachochea wananchi.
Inataka nguvu hizo kulingana na zile za tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC na ile ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma, DPP.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.