Waziri wa ardhi kaunti ya Taita Taveta Mwandawiro Mghanga amewaonya wakaazi katika kaunti hiyo dhidi ya kuuza ardhi ovyo ovyo.
Mwandawiro amesema kuwa katika siku za hivi karibuni wakaazi wengi wamekuwa wakiuza ardhi zao kwa bei rahisi jambo linalowapelekea kusalia na umaskini.
Waziri huyo amesema kuwa baadhi ya wakaazi hao wamekuwa wakinunua na kuuza ardhi pasi na kufuata sheria hitajika kabla ya kufanya hivyo.
Mwandawiro ameongeza kuwa tayari wizara hiyo imeweka mikakati na wizara ya ardhi nchini sawia na tume ya ardhi nchini ili kuona kwamba zoezi la upimaji wa ardhi linafanikishwa ili wakaazi wakapate hati miliki.