Muhuri yakashifu hatua ya kufungwa kwa maeneo ya burudani Mombasa

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI kupitia afisa wa maswala ya dharura katika shirika hilo Francis Auma limeikashifu serikali ya kaunti ya Mombasa kwa kuyafunga maeneo ya burudani ikiwemo fuo za bahari akisema hatua hiyo itazorotesha uchumi wa kaunti hiyo kwa kiwango kikubwa.
Auma amesema serikali ya kaunti hiyo ilipaswa kutafuta njia mbadala za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona bila kufunga maeneo hayo kwani yanachangia katika ukuaji wa uchumi kwenye kaunti hiyo.
Aidha amesema kufungwa kwa maeneo hayo huenda yakachangia kushuhudiwa kwa mambo maovu kwani wengi watabaki bila ajira na kulazimika kushawishika kujiingiza katika uhalifu ili kujikimu kimaisha

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.