Muhiddin asajili ushindi wa kwanza Bandari ikiinyuka Kenya CB 2-1

Mkufunzi Twahir Muhiddin hatimaye amepata ushindi wake wa kwanza katika ligi kuu ya Kenya KPL tangu alipoteuliwa kaimu kocha wa klabu ya Bandari.

Hii ni baada ya kuwanyuka wanabenki Kenya CB magoli 2-1 katika dimba lao la nyumbani la mbaraki.

Bandari ikiwa na alama 23 wanasimama katika nafasi ya 11 huku Kenya CB wakishikilia nafsi ya nne wakiwa na pointi 38.

Hata hivyo kwa upande wao vinara wa ligi kuu na bingwa watetezi Gor Mahia wameendelea kuyumba walilazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji wao western stima ikiwa ni siku chache baada ya kukubali kipigo cha 3-1 mikononi mwa sofapaka

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.