Mudavadi apuuza wito wa kupunguzwa idadi ya kaunti nchini

Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ameapa kutounga mkono kupunguzwa kwa idadi ya kaunti na badala yake kuwataka viongozi wenzake kuhakikisha kwamba ugatuzi unalindwa kikamilifu ili kuafikia malengo ya katiba ya mwaka 2010.

Mudavadi anasema mchakato wa kuandaliwa kwa kura ya maoni inayopendekezwa ni sharti uhusishe wakenya wote na wala sio watu wachache wanaojitafutia nafasi serikalini.

Akizungumza huko Mwatate kwenye kaunti ya Taita Taveta kwenye hafla ya kuchangisha pesa kwa makundi ya wahudumu wa bodaboda, Mudavadi amewataka wanaoshinikiza kupunguzwa kwa idadi ya kaunti kufahamu umuhimu wa ugatuzi mashinani.

Mudavadi aidha ameilaumu serikali akidai kwamba haiangaziii inavyosatahili vita dhidi ya ufisadi huku akimtaka rais Uhuru Kenyatta kutolegeza kamba kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.