MSIMU WA KIANGAZI KUSHUHUDIWA KAUNTI YA KILIFI MWEZI HUU WA JANUARI

Huenda wakaazi wa kaunti ya Kilifi wakashuhudia msimu wa kiangazi mwezi huu wa Januari na siku chache za mvua masaa ya asubuhi.

Haya ni kwa mujibu wa Ramadhan Munga mkurugenzi msimamizi katika idara ya utabiri wa hali ya anga kaunti ya Kilifi ambaye amehoji kuwa zipo baadhi ya sehemu ambazo zitashuhudia mvua nyepesi wakati wa asubuhi wiki hii na kuendelea kushuhudiwa kwa msimu wa kiangazi hadi mwezi wa pili.

Hata hivyo Munga amewaomba wakaazi hasa wale wanaojihusisha na ukulima kuwa tayari kupokea mvua kubwa inayotarajiwa kuanza mwezi Aprili.

Aidha ameitaka serikali kuu kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Kilifi kuweka mikakati kabambe itakayo saidia katika kuhifadhi chakula cha kutosha kwa wananchi wakati wa kiangazi huku akiitaka kitengo kinacho husika na maswala ya dharura kuwa tayari kwani mikasa ya moto huwa inashuhudiwa msimu huu.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.