MSHAMBULIZI TEGEMEO WA BANDARI KUSALIA MKEKANI KWA ZAIDI YA MIEZI 4

Nahodha wa klabu ya Bandari huenda akawa nje kwa miezi 4 akiuguza jeraha alilolipata kwenye mechi dhidi ya Western Stima wikendi iliyopita.

Shaban Kenga alikimbizwa hospitalini baada ya kuumia mguu wa kushoto kufuatia kuchezewa visivyo na Musika Junior katika mechi hiyo ilitamatika kwa magoli 2-0 faida kwa wenyeji Bandari.

Mbali na Kenga wachezaji wengine wa Bandari wanaouguza majeraha ni pamoja na Michael Wanyika William Wadri, Collins Agade, na Abdallah Hassan.

Kenga aliruhusiwa kuondoka hospitalini Jumatano Januari 6 baada ya kufanyiwa upasuaji.

Kwa mjibu wa ripoti ya daktari ni kwamba, nahodha huyo ambaye ni mshambulizi tegemeo kwa Bandari kufuatia kuondoka kwa Wycliffe Ochomo, jeraha hilo litamueka mkekani kwa muda wa miezi mine.

Bandari ambayo ipo mikononi mwa mkufunzi mpya raia wa Rwanda, Cassa Mbungo, itamenyana na Zoo FC wikendi ijayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.