MPANGO WA KUWALIPIA KARO WANAFUNZI WALIOKOSA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU WAANZISHWA ENEO BUNGE LA MAGARINI

Wazee wa vijiji eneo Bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wameanzisha mpango wa kulipia karo wanafunzi waliokosa kujiunga na vyuo vikuu licha ya wao kuhitimu masomo ya sekondari eneo hilo.
Wakiongozwa na Hamadi Chad Karisa ambae pia ni mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha Federal Party of Kenya amesema kuwa mpango huo unaofahamika kama ELIMIKA KWA WOTE unajumuisha wanajamii wote kama washikadau jumuku kuu ikiwa kutoa ufadhili wa masomo kwa kushirikiana na jamii kufanya michango.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa hatua hiyo ilijiri baada ya wanajamii kubaini kuwepo kwa wanafunzi waliohitimu masomo ya sekondari na kukosa kujiunga na vyuo vikuu kufuataia hali ya uchochole inayo wakumba majumbani mwao.
Hata hivyo Chad Karisa ameeleza uhakika wa mpango huo kuzaa matunda katika jamii kwa kile alichokisema kuwa wananuia kuhusisha kamati ya hazina ya CDF kwa kuwasilisha majina ya wanafuzi ambao watakuwa wamenufaika na mpango huo katika eneo la Magarini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.