Michael Kingi awahimiza wenyeji wa Magarini kuwapeleka watoto wao shuleni

Mbunge wa Magarini kaunti ya Kilifi Michael Kingi amewahimizwa wazazi katika eneo hilo kukumbatia agizo la serikali la kuwapeleka watoto wao waliomaliza darasa la nane kujiunga na kidato cha kwanza.
Katika hotuba yake kwenye hafla ya kupeana ufadhili wa madawati kwa shule ya msingi ya Karimboni wadi ya Garashi amesema wazazi hawapaswi kutoa sasabu zozote za kutowapeleka watoto wao kujisajili na kidato cha kwanza.
Kingi amesema kaunti ndogo ya Magarini imebahatika kuwa na shule nyingi za upili ikilinganishwa na eneo bunge la Malindi licha ya kuwa na changamoto ya uhaba wa walimu na madarasa lakini tayari serikali kuu imeweka mipango ya kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa.
Aidha, amewataka wazazi kufika katika ofisi yake pindi tu matokeo ya mtihani wa darasa la nane yanapo toka ili kujiandikisha kwa kutuma maombi ya ufadhili wa masomo kwa mashirika na kampuni zinazo nuia kuwafadhili wanafunzi wasioweza kujikimu kifedha ili kupata elimu.
Hata hivyo ameahidi kujenga maabara kwa kila shule ya upili eneo bunge la Magarini ili wanafunzi wapate elimu bora na pia sekta hiyo iweze kuimarika.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.