Mchekeshaji Idris Sultan aripoti polisi Dar leo

Mchekeshaji maarufu raia wa Tanzania Idris Sultan leo Ijumaa Novemba 1,  asubuhi ameripoti Kituo cha Polisi ‘Central’ jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya masharti ya dhamana aliyopatiwa jana October 31, 2019.

Sultan alitakiwa kwenda polisi baada ya kuweka picha yenye sura yake huku akiwa ameketi katika kiti chenye nembo ya Taifa na kuambiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuripoti kituo chochote cha Polisi.

Mchekeshaji huyo pia, aliweka picha nyingine inayoonyesha sura ya Rais John Magufuli akiwa amesimama huku amevaa suruali yenye mikanda inayoshikizwa mabegani maarufu kama suspender.

Rais Magufuli alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa anafikisha umri wa miaka 60 Jumanne wiki wiki hii.

Muda mfupi baada ya kuchapicha posti yake Sultan, akaunti ya mtandao wa Instagram inayodhaniwa kuwa ya kamishna wa kanda ya Dar es Salaam, Paul Makonda, ilichapisha posti picha moja ya alizoposti Sultan na kuandika akimwambia mchekeshaji huyo ajisalimishe katika kituo cha polisi kilicho karibu naye.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.