Mawasco yalalamikia wizi wa mita za maji

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kusambaza maji mjini Malindi kaunti ya Kilifi MAWASCO Gerald Mwambire amelalamikia wizi wa mita za maji.
Mwambire amesema hatua hiyo huenda ikaathiri utoaji huduma katika jamii hususan wakati huu wa janga la Corona.
Aidha, amehoji kuwa huenda wanaotekeleza wizi huo wanaziuza mita hizo kwa bei ya reja reja kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.
Wakati uo huo ameongeza kwamba kuanzia wiki ijayo visima viwili vitakuwa vimekarabatiwa na huenda sasa tatizo la uhaba wa maji ambao umekuwa ukishuhudiwa mara kwa mara likapata suluhu la kudumu.
Awali kampuni hiyo ilibainisha kuwa uhaba wa maji eneo ulikuwa unatokana na uharibifu wa visima kadhaa vya maji katika kituo kikuu cha kusambaza maji cha Baricho.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.