Matsangoni kaunti ya Kilifi yaidhinishwa rasmi kuwa wilaya

Ni afueni kwa wakaazi wa eneo bunge la Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi baada ya eneo la Matsangoni kuidhinishwa rasmi kuwa taarafa katika eneo bunge hilo.
Akizungumza na meza yetu ya habari kwa njia ya simu mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amesema kuwa kumekuwa na ugumu wa maafisa wa utawala kutekeleza huduma zao kwa wananchi.
Owen amehoji kuwa baadhi ya maswala ambayo wamezingatia katika kutekeleza hilo ni kwepo kwa taasisi za elimu za kutosha kwenye sehemu hiyo na hata vituo vya afya ambavyo vitasadia katika kuwahudumia wenyeji huku wakiweka vituo vya polisi katika kila wilaya kwenye sehemu hiyo.
Hata hivyo, mbunge huyo amewahakikishia wakaazi wa eneo la Gede kuwa wako katika harakati za kuhakikisha kuwa wakaazi wa eneo hilo wanapata kituo cha polisi pamoja na naibu kamishna sambamba na afisi zingine ili kuboresha huduma bora kwa wananchi hao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.