Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu pwani yataka uchunguzi wa mauaji ya Mohammed Mapenzi kuharakishwa

Mashirika ya kautetea haki za kibinadamu kanda ya pwani yameelezea kughadhabishwa na namna serikali inavyoendesha kesi za mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na maafisa wa usalama.
Yakiongozwa na mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Hussein Khalid yanaitaka serikali kuharakisha uchunguzi wa kesi ya Mohammed Mapenzi ambaye aliuawa na watoto wake wawili huko Kibundani kaunti ya Kwale.
Kwa mujibu wa wanaharakati hao ni kuwa imekuwa changamoto kubwa kwao katika kutafuta haki kwa waasiriwa na hata baada ya kutafuta usaidizi kwa asasi za usalama hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuhusiana na uchunguzi huo.
Wameongeza kuwa uchunguzi huo umechukua muda mrefu na huenda familia ya Mohammed Mapenzi ikakosa kupata haki.
Mauaji hayo yalitokea tarehe 25 mwezi wa Tano mwaka huu huku Familia ya marehemu ikisisitizia haja ya kupata haki kama wakenya wengine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.