marufuku ya kuingia na kutoka Eastleigh na Mji wa Kale yaongezwa hadi Juni 6.

 

Watu 66 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona na idadi ya maambukizi kufikia 1029.
Katika taarifa yake kwa wanahabari akitoa takwimu kuhusu maambukizi hayo waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema idadi hiyo ni ya juu zaidi kutangazwa kwa kipindi cha saa 24 zilizopita.
Kufuatia ongezeko la maambukizi hayo sasa wizara hiyo imesema mikahawa itasalia kufungwa huku marufuku ya kuingia na kutoka eneo la Eastleigh jijini Nairoibi na Mji wa Kale katika kaunti ya Mombasa ikiongezwa hadi Juni 6.
Kulingana na taarifa hiyo kaunti ya Mombasa inaongoza kwa visa vipya viliyotangazwa leo ambapo ni 30 na Nairobi 26.
Kagwe amesema serikali ya Kenya imepokea msaada wa maabara tamba kutoka ubalozi wa Ujerumani ili kuimarisha zoezi la kuwapima madereva ambao wanasafirisha mizigo.
Hii ni baada ya Ujerumani kutoa msaada wa maabara tamba 9 kwa mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki huku Kenya ikipokea maabara 2.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.