MAN UNITED WAPEPETWA NA CITY 2-0

Mashtenai wekundu kwa mara ya nne wametemwa nje ya michuano ya Carabao baada ya kupoteza 2-0 mikononi mwa Manchester ugani Old Trafford.

Magoli kutoka kwa John Stones na Fernandinho dakika za lala salama ya mchezo yalitosha kuwapa nafasi kwenye fainali ya Kombe la EFL ambapo itawakutanisha mahasidi wa zamani Jose Mourinho na Pep Guardiola.

Katika mchezo wa matao ya juu, Citizens walionekana kuwa na mshawasha na kucheza kwa mtindo wa uledi ambao ulitatiza sana safu ya ulinzi ya Manchester United.

Walitingisha wavu mara mbili lakini mabao yao yote yalikataliwa kwa kuotea, huku Kevin De Bruyne pia akigonga mwamba.

Mapema katika awamu ya pili, masogora wa Pep Guardiola walichukua uongozi baada ya mlinzi John Stones, ambaye hatima yake Manchester City yayumba, kupachika mpira wavuni kutokana na frikiki ya Phil Foden.

United walilemewa kwenye mchezo huo dhidi ya mahasimu City ambao walitawala na kuwazuia kuingia kwenye ngome yao kupitia kwa kiungo Ruben Dias.

Mashetani Wekundu walijaribu kutafuta bao la kusawazisha lakini City waliweka mwanya kubwa kwenye mchezo huo huku Fernandinho akitia kimyani pasi ya Dean Henderson baada ya utepetevu kwenye upande wa United.

United walimshirikisha sajili Donny Van De Beek dakika za lala salama lakini mzawa huyo wa Uholanzi alishindwa kuleta tofauti kwani tayari muda ulikuwa umeyoyoma.

Mara ya mwisho United kupoteza mechi ni wakati Leipzig waliwatema nje ya Ligi ya Mabingwa na sasa Solskjaer amefungiwa nje tena na mahasidi City.

Akizingumza baada ya mechi hiyo, Solskjaer alikubali kushindwa na City akikiri kuwa kikosi chake kilishindwa maarifa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.