Makampuni na Viwanda kufungwa kaunti ya Kilifi

 

Serikali ya kaunti ya kilifi imetoa agizo la kufungwa kwa makampuni na viwanda vyote katika kaunti hii kwa muda usiojulikana kufuatia visa vya virusi vya Corona.
Haya ni Kwa mujibu wa katibu wa serikali ya kaunti ya Kilifi Mkare Jefwa kupitia barua iliyotumwa kwa vyombo vya habari hatua ambayo imechukuliwa kufuatia kuripotiwa kwa visa vya virusi hivyo siku chache baada ya naibu gavana wa Kilifi Gedion Saburi kupatikana na virusi hivyo.
Baadhi ya Viwanda na Makampuni ambayo yatasalia kufungwa ni zile za Saruji ya Mombasa, zile za kutengeneza chumvi na za uvunaji mchanga miongoni mwa zingine katika kaunti ya Kilifi.
Aidha serikali ya kaunti hii imetoa ilani kwa makampuni ambayo yatakiuka agizo hili kuwa yatachukuliwa hatua kali za kisheria.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.