Mahakama yamuachilia kwa dhamana Swazuri

Aliyekuwa mwewnyekiti wa tume ya kitaifa ya ardhi Daktari Mohamed Swazuri pamoja na wenzake watano wanaostakiwa kwa tuhuma za ufisadi wameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja au bondi ya shilingi milioni thelathini.

Uamuzi huo umetolewa na hakimu mkuu Lawrence Mugambi baada ya kukana mashtaka yanayowakabili ikiwamo matumizi mabaya ya ofisi, Ufisadi, Ulanguzi wa fedha miongoni mwa mashtaka mengine.

Ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa kamishna Emma Njogu, aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Tom Chavange na katibu wa tume Lillian Kaverenge.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.