Mabwenyenye wanaopora ardhi za wenyeji wa pwani waonywa vikali

 

Migogoro ya ardhi inaendelea kushuhudiwa kanda ya pwani na kutajwa kuwa donda sugu huku Mabwenyenye walio na tabia ya kuvamia na kupora ardhi za wenyeji wakionywa vikali.
Haya yanajiri huku Kamati ya usalama katika kaunti ndogo ya Kilifi kusini ikiwataka mabwenyenye hao kusitisha hulka ya kuvamia na kupora ardhi hizo eneo la pwani kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Kulingana na naibu kaunti kamishna katika eneo la Kikambala eneo bunge la Kilifi kusini Ahmed Mahmoud amesema kuwa kuna makundi ya vijana ambayo yanatumiwa kupora ardhi za watu katika eneo hilo bila kujali wenyeji walio na hati miliki.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.