Maandalizi ya Afcon: Harambee Stars kuelekea Ufaransa leo Taifa Stars wakiingia kambini kesho Jumamosi

Kocha wa Harambee Stars ya Kenya Sebastian Migne ameita wachezaji 27 kuunda kikosi cha timu ya taifa ya Kenya kitakachoshiriki michuano hiyo. Harambee Stars itaondoka leo Ijumaa kuelekea Ufaransa kwa kambi ya wiki tatu.

Upande wa majirani zao, timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaingia kambini kesho jumamosi katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam kujiandaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) baadaye mwezi huu nchini Misri.

kambi hiyo ya awali ya wiki moja kwa maandalizi hayo hadi Juni 7 kisha itasafiri kwenda Misri kwa michuano ya AFCON.

Harambee na Taifa Stars wamepangwa kwenye kundi moja la C pamoja na Senegal na Algeria. Michuano ya AFCON imeratibiwa kuanza Ijumaa Juni 21 na kukamilika Ijumaa Julai 19. 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.